HABARI


KANSA YA NGOZI YAUA ALBINO
Katibu wa Chama cha Walemavu wa Ngozi mkoani Tanga, Mahamoud Salehe, amesema  kuwa walemavu wa ngozi watano wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa kansa uliosababishwa na kukosa losheni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

 Salehe amefafanua kuwa ugonjwa wa kansa ya ngozi ni tishio kwa maisha ya walemavu hao ambao kila mwaka miongoni mwao, wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa tiba baada ya kuugua.

Aidha, amesema changamoto nyingine zinazowakabili albino mkoani Tanga ni pamoja na ukosefu wa kliniki ya kudumu ya ngozi wilayani, ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya ualbino kwa jamii na albino wenyewe na walimu kutokuwa na elimu maalumu kuhusu changamoto za albino waliopo shuleni.




WANAFUNZI DSJ WATEMBELEA KITUO CHA YATIMA


 Mratibu wa masomo wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji (DSJ) Joyce Mbogo amesema jamii inapaswa kujitoa na kuwasaidia watoto yatima kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa na wanahitaji faraja kutoka kwa jamii inayotuzunguka. 
akizungumza na mwandishi wa habari katika kituo cha kulelea watoto yatima cha msimbazi center kilichopo ilala jijini dar es salaam amesema kuwa kujitoa ni jambo la kheri kwani kunawafanya watu kuwa karibu na jamii kwa kuwatembelea na kuwafariji.
"tunaishi kwenye jamii nasi pia yatupasa kuwakumbuka wanajamii wanaotuzunguka kwa kujitoa na kutoa kile kilicho ndani ya uwezo wetu kwa kuwa ni jambo jema na kuleta upendo wa kweli kwa jamii" alisema Mbogo.
Naye mlezi wa watoto wa kituo cha msimbazi Center amewashukuru wanafunzi wa DSJ kwa kuwatembelea na  amewataka wazazi wasiwahukumu watoto kwa kuwatelekeza na kuwataka wawe na malezi mazuri kwa familia yao.






UTEUZI MAWAZIRI DSJ MOSHI MWEUPE.
Na, Mwandishi wetu
Dar es salaam,

Raisi wa chuo cha uandishi wa habari Dar-es-salaam(DSJ). Lunyamadizo Mlyuka amewataka wanafunzi katika chuo hicho kuwa wavumilivu wakati wakisubiri uteuzi wa baraza la mawaziri na wajumbe mbali mbali katika serikali yake.
  
   Akizungumza na gazeti letu Mlyuka amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya DASJOSO uteuzi wa mawaziri na wajumbe unatakiwa kufanyika baada ya wiki mbili toka Rais kuapishwa.

Pia amesema anataka  kuwepo na baraza la mawaziri lenye ushirikiano na kila mwanafunzi katika chuo hicho.

“Tunahitaji baraza lenye ushirikano utakao simama kwa ajili ya masilahi ya wana DSJ na kusimamia vyema katiba ya DASJOSO bila kuvunja katiba ya Nchi “ alisema Mlyuka.
  
Hata hivyo Rais amewataka wanafunzi kufanya kazi kwa ushirikiano na kusoma kwa bidii ili kupata heshma na ushindi wa kishindo ambapo hakuwa na mpinzani. Katika uchanguzi huo uliofanyika September 9 mwaka huu. Mlyuka alipata kura za ndio 237 na hapana 35 huku kukiwa hakuna kura zilizoharibika.
  
Uchaguzi DASJOSO hufanyika kila mwaka ambapo mwaka jana alichaguliwa Ibrahimu Ibrahimu lakini alipinduliwa baada ya ofisi yake kumtuhumu kuwa kulikuwa na ubadilifu wa fedha na kuchaguliwa Raisi wa mpito hadi ulipofanyika uchaguzi mkuu mwezi huu.




MLEZI AFUNGUKA KUHUSU MAADILI YA MAVAZI.

Na Tabia Mkilwa
 Dar-es-Salaam,

Mlezi wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (DSJ) Joachim Joliga amewaonya  wanafunzi  kutokuvaa mavazi  Yasiyo kuwa na maadili ya nidhamu chuoni hapo.

Amezungumza hayo chuoni hapo katika viwanja vya Basata na kusema kuwa changamoto ni nyingi anazokumbana nazo kutokana na wanafunzi  kutokuwa makini na kutozingatia wengi wao hutumia njia za panya kuingia chuoni nakutokuwa na nidhamu.

“ mwanafunzi yeyote atakaye kiuka maadili ya katiba ya serikali ya wanafunzi DASJOSO atapata adhabu kari ya kinidhamu nay a maadili mabaya “ alisema Joliga.
Bashir Musa amesema ni jambo zuri kwani linakuza maadili na pia huongeza heshima ya chuo kati ya walim na wanafunzi ili kutengeneza muonekano mzuri na mazingira wa chuo hicho.

 Naye Warda Kikoti amesema ni jambo zuri kuweka maadili mazuri kuhusu mavazi kwani wengi wao huwa hawaelewi mavazi yapi yanayotakiwa lakini bado hawaelewi wanavaa wengine kama wanaenda disco mimi nimeshukuru hii hali ya kukatazwa zaidi kama kutakuwa na sare ya mavazi ili kuleta muonekano mzuri kwa wanafunzi.
 




 WAFANYABIASHARA WAMEPEWA SIKU SABA KUHAMA BARABARANI

dcc temke


Na Tabia Mkilwa

Dar es salaam

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva amewataka wafanyabiashara ndogondogo (machinga) wanaofanya biashara Mbagala Rangi tatu kando ya Barabara ya Kilwa na Bias amewapa siku saba ili  waende kwenye masoko waliyopangiwa na wenye maeneo kwenye masoko warudi  mara moja .


Hayo amezungumza alipotembelea stendi ya mabasi yaendayo wilaya ya mkoa wa pwani mbagala jijini dar es salaam jana na kusema kuwa wafanyabiashara wote wa barabarani warudi kwenye maeneo waliyopangiwa na serikali .

"wafanyabiashara wanaopanga kando ya barabara waondoe bidhaa zao kuanzia leo kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa mapema " alisema Lyaviva.

Pia amesema stendi ya mabasi yaendayo wilaya mkoa wa pwani inayomilikiwa na mtu binafsi Maulid Shabani amesema mabasi hayo yakaungane na stendi ya Mjini kwa muda wa siku kadhaa .

"mabasi yote yaendayo pwani yakaungane na stendi ya mjini mapema ili kuepusha msongamano wa mabasi na abiria " alisema Lyaviva.

Naye mmoja wa wananchi Robert Daniel amesema hatua hizo ni mzuri ila eneo halitoshi kwa sababu ya uwingi wa mabasi na abiria kwani kutasababisha msongamano wa watu kuwa wengi na kuongeza vibaka.

No comments:

Post a Comment