MICHEZO

farid-musa-10

 Uchunguzi uliofanyika umebainisha kuwa, habari iliyotoka Azam FC kuhusu kupokea kibali cha kazi cha Farid Musa si za kweli badala yake wamepokea form ya kuombea kibali hicho.

Wakala wa Farid Musa, John Sorzano amekanusha habari zilizozagaa kuwa tayari kibali cha kazi kimeshatoka na badala yake amesema hicho kilichotapakaa kwenye mitandao ya kijamii si kibali ni form ambayo itatumiwa katika mchakato wa kuombea kibali.

 Solzano ameshangaa form hiyo kutapakaa mitandaoni wakati ni kitu cha siri huku akisisitiza kuwa, wametumiwa Azam na yeye lakini kwa upande wa Tanzania, tayari form hiyo imeshaonekana kwenye mitandao ya kijamii Kitendo cha hiyo form kusambaa mitandaoni huenda kuhatarisha Farid kupata kibali cha kazi.

“Hii form nimetumiwa mimi pamoja na klabu ya Azam, lakini nashangaa wao wameiweka mitandaoni wakati ni kitu cha siri, kwa upande wangu mimi nilifanya kuwa siri. Farid sio kwamba amepata kibali lakini mchakato bado unaendelea,” anasema John Sorzano wakala wa Farid Musa.

 

Alikiba: Sipendi kiki na sitofanya kamwe

 Hitmaker wa ‘Aje’ Alikiba amesema Kiki ni kitu ambacho hakipo kwenye menu yake.

14716444_1139160262829024_4134658599454507008_n
Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Clouds 30 kupitia Clouds TV.
Kwanza kwangu mimi hicho kitu hakipo, sijui kusema mimi nina hela. Na kuna watu wengine wanaongopa kwa kusema uongo tu kwasababu watanzania tumeshakubali kupelekwa na hiyo,” alisema.
“Lakini kuna baadhi pia ya watanzania wapo makini sana, huwa hawakubali kitu kirahisi na kuna wengine ni wepesi sana kuamini. Na hizi kiki zinakuja kwasababu watu wanaamini. Mimi binafsi sitaki kabisa hivyo vitu na sitokuja kufanya na kama kuna watu wanafanya hivyo vitu mimo nimewaambia unajua kila mtu ana identity yake kwamba hawa ni watu wa aina hii na hawa ni hii.”
Ukiongea kitu mtu mwenye akili zake timamu anajua kabisa hii si kweli na Alikiba hawezi kufanya hivyo. Ila huyu anaweza kufanya hivyo na huyu hawezi kufanya hivyo ila Alikiba anaweza fanya hivyo,” alisisitiza.


jembe la arsenal latua crystal palace


Kiungo wa zamani wa Arsenal, Mathieu Flamini amejiunga na Klabu ya Crystal Palace akiwa mchezaji huru. 


  Flamini ambaye alitwaa mataji matatu ya FA akiwa na Arsenal alipokuwa akionekana ni mzuri kwenye kiungo cha ukabaji, pamoja na ubingwa wa Serie A alipokuwa AC Milan, amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Flamini aliondoka Arsenal baada ya kucheza mechi 246 katika awamu mbili, anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Palace msimu huu.


Wengine waliosajiliwa na Palace msimu huu ni Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins na Christian Benteke huku Loic Remy wa Chelsea akitua kwa mkopo.

..................................................................................................................................



Staa wa zamani wa Barcelona, Xavi amesema kuwa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni mchezaji mzuri laini anachokosea ni kujifananisha au kuzaliwa katika utawala wa Lionel Messi wa Barcelona.
   

Upinzani baina ya Ronaldo na Messi umekuwa mkubwa na umedumu kw amiaka kadhaa katika soka la Ulaya kwa kuanzia kwenye La Liga huku wawili hao wakiwa wametwaa tuzo nane za Ballon d’Or katika miaka nane iliyopita.











Ronaldo na Xavi wakatihuo Ronaldo alipokuwa Manchester United.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri kwa nafasi yake, tatizo ni kuwa kuna mwingine ambaye ni bora kwenye historia ya soka na anaendelea kucheza.

“Ronaldo ni kifaa lakini kumfananisha na Messi, kwangu mimi na kwa mtu anayejua soka ni vitu vitiwili tofauti.

“Messi ataendelea kuwa namba moja kwa muda wote mpaka atakapoona inatosha, ni mchezaji bora labda uwe shabiki wa Real Madrid ndiyo unaweza kukataa,” alisema Xavi ambaye kwa sasa anaichezea Al Sadd SC ya Doha.


No comments:

Post a Comment